Video: Alice Kimanzi - Waambie | Mp4 Download

Video: Alice Kimanzi - Waambie | Mp4 Download

WAAMBIE LYRICS:
Usingizi kanitoroka moyoni nakesha ngoma, Kwa subira nimengoja penzi hili la thamana, Tangu tulipokutana nafsi zetu kapatana, Na ni mbali tumetoka tangu kuchumbiana, Siku yetu imefika hakuna 'taye zuia, Ajalie Maulana pete tutavishana,

Waambie mie nimeshapatikana, Na yule mume wa mapenzi 'sha nienzi, Waambie mie milele nishazama, Sinitafute kule kwa mabinti nishahama,

Angalia Ishara {Angalia} Tazama Ishara {Angalia} Angalia Ishara {Angalia} Mi nishahama {Mi nishahama} Angalia Ishara {Angalia} Tazama Ishara {Angalia} Angalia Ishara {Angalia} Mi nishazama {Mi nishazama}

Kuna wale wanasema ndoa haidumu tena, Yaje maji na mafuriko tayari tushatia nanga, Nimempata yule wangu kampenda na vyote vyangu, Sitajasahau amenivisha dhahabu, Nimempata yule wangu kampenda na vyote vyangu Simulia walimwengu nishampa moyo wangu,

Waambie mie nimeshapatikana, Na yule mume wa mapenzi 'sha nienzi, Waambie mie nishazama, Sinitafute kule kwa mabinti nishahama,

Angalia Ishara {Angalia} Tazama Ishara {Angalia} Angalia Ishara {Angalia} Mi nishahama {Mi nishahama} Angalia Ishara {Angalia} Tazama Ishara {Angalia} Angalia Ishara {Angalia} Mi nishazama {Mi nishazama}

Ee Mola tusaidia kwa wema wako, Tuwe na ndoa yenye furaha, Milele hadi milele

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog